Rochdale Rotary Club
Rochdale Masonic Buildings
Richard Street
Rochdale
OL11 1DU
contactus@accessible-edibles.org

ORODHA YA KUZINGATIA KATIKA MRADI MPYA WA URBANFARM

Marejeleo yote, kwa mfano, FIG 6 inarejelea picha kwenye Mwongozo wa UrbanFarm.

Ni MUHIMU usome huo mwongozo kabla ya kuanza mradi wako.


 1. KUCHAGUA MIFUKO

 2. Angalia ifuatayo yanapatikana:

  1.1 - Mifuko ya plastiki ya kubebea bidhaa kutoka kwenye Supermarket (Angalia FIG 6 & 7)

  1.2 - Mifuko ya saruji ya zamani, lakini sio karatasi (Angalia FIG 5)

  1.3 - Mifuko yoyote ya turubai (Kanvasi)

  1.4 - Vazi lililotupwa linawezashonwa kutengeneza begi (ona FIG 9)

  1.5 - Ikiwa unatumia mifuko ya nguo kama vile 1.4, weka begi nyembamba ya plastiki au karatasi ndani kupunguza upotezaji wa maji.

  1.6 - Bomba au tubu ya plastiki au vifaa vilivyoshonwa kwenye sura ya tube (Tazama FIG 2)

  1.7 - Kumbuka ikiwa una eneo ndogo sana la UrbanFarm yako, zingatia saizi ya mifuko yako ndio iweze kutoshea kwa nafasi uliyo nayo. 3. KUAMUA KIWANGO CHA UREFU UTAKAOPACHIKA MIFUKO

 4. 2.1 - Ikiwa eneo linaweza kufurika, weka mifuko juu ya urefu wa kiwango cha kawaida cha mafuriko.

  2.2 - Ikiwa mafuriko ya kawaida na yanayotabirika yatoka kwa maji ya bahari, na ardhi itabaki iliyochafuliwa kwa muda mrefu baadaye, hifadhi mifuko, mbolea na mbegu. Hii itaruhusu wakulima wa kawaida kuanzisha ukulima wa UrbanFarm mpaka ardhi yao itakapofaa kutumika tena.

  2.3 - Ikiwa kuna mifugo jaribu kuweka mifuko juu ya urefu ambao wanaweza kufikia.

  2.4 - Ikiwa watoto au walemavu watatumia mifuko hiyo, iweke kwa urefu ambao wanaweza kufikia. 5. UTAKAVYOWEKA MIFUKO

 6. 3.1 - Tafuta ukuta au uzio utakaotumia kuning'iniza mifuko (Tazama FIG 1 & 3).

  3.2 - Ikiwa utapachika mifuko kwenye ukuta au uzio, jaribu kuchagua eneo ambalo jua na kivuli zitafikia kiwango unachotaka.

  3.3 - Tafuta miti inayoweza kutumiwa kuning'iniza mifuko.

  3.3.1 - Mifuko inaweza kuning'inizwa kwenye matawi ya miti (Tazama FIG 4).

  3.3.2 - Mifuko inaweza kupachikwa kwenye shina la mti kwa kamba iliyofungwa kwenye mti.

  3.3.3 - Mifuko inaweza kupachikwa kwenye kamba iliyofungwa kwenye miti miwili au zaidi.

  3.3.4 - Ili kuongezea idiadi ya mazao, kamba mbili zilizowekwa sanjari kati ya miti miwili inawewezatumiwa, lakini, hakikisha unaweza kufikia salama kamba iliyo juu na mifuko yake. Wazo hili ni sawa na FIG 5 lakini ukitumia kamba kati ya miti badala ya miti ya mianzi.

  3.3.5 - Mwishowe ikiwa hakuna kitu kinachopatikana kwa urahisi kwenye eneo lako, tafuta kitu chochote ambacho kinaweza kubadilishwa kushikilia mifuko hiyo, kwa mfano jengo lisilotumika au au gari chakavu iliyotupwa au chochote. Mawazo yako daima yatakusaidia kupata suluhu.

  3.4 - FREMU ZA KUPACHIKIA MIFUKO. Ikiwa hauna miti, ua, au ukuta kwenye eneo lako la UrbanFarm aunaweza kutengeneza fremu na kuzitumia. Ikiwa una saruji, au ardhi yenye mawe ambayo haitumiki au paa thabiti ya simiti ambayo ina nguvu ya kutosha kubeba uzito wa idadi kubwa ya mifuko, inaweza kutumika lakini utahitaji kutengeneza fremu za kupachika mifuko ya ukulima.

  3.4.1 - Ikiwa hauna mbao za zamani ambazo zinaweza kutumiwa, itabidi kununua mbao, na hii itakuwa bei ghali zaidi kwa chaguzi zote.

  3.4.2 - Ikiwa una sehemu ya ardhi isiyo ngumu, kutengeneza fremu kwa urahisi itabidi kushindilia mbao mbili kwenye mchanga (vikingi), na ingine moja ikiunganisha hizo mbili kama lengo ya mpira. Mifuko inaweza kuninginizwa kwenye mbao inayoshikanisha vikingi viwili.

  3.4.3 - Ikiwa sehemu ya ardhi uliyo nayo ni ngumu, itabili utengeneze fremu kikamilifu ikiwa na msingi wake. Tazama FIG 7. 7. MBOLEA

 8. 4.1 - Angalia kinachopatikana kwenye eneo lako.

  4.2 - Ikiwa utapachika mifuko kwenye ukuta au uzio, jaribu kuchagua eneo ambalo jua na kivuli zitafikia kiwango unachotaka.

  4.3 - Ikiwa italazimika kununua mbolea ya kuanza mradi ,himiza UrbanFarmers wako kutengeneza mbolea yao wenyewe. Hii itasaidia kukuza upanuzi wa baadaye.

  4.4 - Angalia ikiwa kuna UrbanFarmers wa kutosha kuanza huduma ya kutengeneza mbolea kwa pamoja. 9. KUWEKA KIVULI

 10. 5.1 - Ikiwa jua ni kali sana kwa mimea, unawezaweka kadibodi, vipande vyeusi vya plastiki, au mabati juu ya eneo unayoweka mimea yako ili kuikinga kutokana na jua kali au mvua.

  5.2 - Ikiwa kuna uwezekano wa mvua kubwa hakikisha mifuko ya hii mimea imefungwa hapo juu kwa kutumia pegi za nguo au imefunikwa kwa njia iliyoelezwa 5.1 hapo juu 11. UWEZEKANO WA BIASHARA

 12. 6.1 - Chunguza kama kuna watu wa kutosha kwenye maeneo ambao wanawezaunda kikundi cha kujisaidia.

  6.2 - La kipaumbele itakuwa ni kukuza chakula cha kutosha ili watu wawe na chakula cha kutosha.

  6.3 - Ikiwa unayo nafasi ya kuongeza mifuko zaidi, zingatia uwezekano wa kukuza vyakula zaidi vyenye thamani kubwa, ili vingine vinaweza kuuzwa.

  6.4 - Ikiwa kuna nafasi ndogo tu ya kuweka mifuko yako, zingatia kupanda mazao yenye thamani kubwa ya kuuza, kisha, tumia faida kununua vyakula vya msingi.

  6.5 - Zingatia kupanda vyakula vyenye ya bei ya juu kama vile pilipili, stroberi au vingine vyovyote ambavyo ni ghali kununua sokoni.