Rochdale Rotary Club
Rochdale Masonic Buildings
Richard Street
Rochdale
OL11 1DU
contactus@accessible-edibles.org

FAIDA ZA URBANFARM

  1. Bei ya chini sana na bora kwa matumizi katika nchi zinazoendelea.

  2. Ni hai, hutumia maji kidogo na ni sawa kwa ukuzaji wa mboga na matunda haswa kwenye ukame.

  3. Inaweza kuwa chanzo muhimu cha vyakula kwa Mkulima wa Mjini. Ikiwa kuna mazao ya gharama kubwa kama vile pilipili au Stroberi yanaweza kupandwa na kuuzwa kutoa pesa kwa familia kununua vyakula vya msingi.

  4. Unaweza kuhisi Mizizi ya mimea kwa urahisi kila siku kuangalia hali ya unyevu ndio ujue wakati wa kunyunyuzia maji.

  5. Chakula kinaweza kupandwa bila shamba, eneo lolote la mjini au vijijini ambalo kunyongwa mifuko itakuwa nzuri.

  6. Hutumia mifuko inayopatikana kwa urahisi kwa mfan: mifuko ya kununulia bidhaa, mifuko ya saruji (lakini sio ile karatasi) au pia begi ya kitambaa ikitumika pamoja na mfuko mwembamba wa plastiki uliowekwa ndani ili kupunguza upotezaji wa maji.

  7. Ni mfumo rahisi kuelewa na una ajira bora kwa wafanyikazi wasio na ujuzi, na unawezakutumila kama zana ya kufundisha shuleni au vyuo vikuu.

  8. UrbanFarm inaweza kusanikishwa juu ya uso wowote kama vile simiti, jiwe, au kwenye paa la simiti kwa gorofa yenye nguvu ya kutosha kubeba uzito wa mifuko, kwenye miti, ukuta, kwenye kamba (kama ya kuanikia nguo), au kwenye ardhi iliyochafuliwa kufuatia mafuriko au shamba lenye mchanga usiofaa ukulima n.k. Ukitaka kuongeza mazao weka safu kadhaa za mifuko iliyopachikwa wima.

  9. Hutumia vifaa vinavyopatikana kwa urahisi tena kwa gharama ya chini. Vifaa vyovyote vinaweza kubadilishwa ili kufanya kazi: kwa mfano mchanga wa mtoni, manyoya ya nazi au magazeti ya zamani kwenye mbolea. Kwa vile gharama ya kuanzisha mradi iko chini, UrbanFarm inaweza kubadilisha maisha ya watu masikini duniani.

  10. Kwa vile hii mifuko hupachikwa juu, inazuia vyakula kuharibiwa na wanyama na mifugo kama ngombe, mbuzi, sungura na pia huzuia wadudu wa ardhini kama vile konokono.

  11. Urefu wa mifuko unafaa kuzingatia ufikiaji kwa wakulima walemavu, watoto na wazee.

  12. Ukulima wa UrbanFarm unaweza kutoa mazao ambayo yanaweza kuuzwa kibiashara.

  13. UrbanFarm husaidia haswa wanawake kujitegemea, inahimiza watu kufanya biashara, na pia inaweza kusaidia katika kusaidia maafa.