Rochdale Rotary Club
Rochdale Masonic Buildings
Richard Street
Rochdale
OL11 1DU
contactus@accessible-edibles.org

KUFADHILI MRADI WAKO

Mradi wetu wa UrbanFarm ® ulitengenezwa kwa madhumuni ya kulisha maskini ambao hawana chakula cha kutosha kula, na hii itakuwa kipaumbele chetu siku zote.

Walakini kazi yetu ya maendeleo ya mradi imetufundisha kwamba mara tu mahitaji ya kimsingi ya wanadamu ya chakula yatatoshelezwa, kuna fursa nzuri ya ukuaji na mauzo ya faida ya mboga na matunda.Hii inasaidia haswa wanawake kujitegemea kiuchumi.

Inaweza kuchukua njia mbili tofauti. Kwanza vyakula vya kawaida au mazao ya msingi yanaweza kupandwa na kuuzwa, au, mazao ambayo ni ghali kununua katika soko yanaweza kupandwa na kuuzwa, na faida kutumiwa kununua vyakula vya kawaida vya kulisha mkulima wa UrbanFarm.

Kwa hivyo, mashirika ambayo inahusika katika kuanzisha UrbanFarms katika jamii zao yanaweza kuchagua kutumia mchanganyiko wa mazao na kukuza mazao ya kula na ya kuuza.

Tukizingatia haya, mashirika yanapaswa kuzingatia kwa uangalifu kwamba punde tu watu wamepata chakula cha kutosha, yanaweza kuanzisha UrbanFarm® ambayo tayari ni operesheni ya gharama ya chini, na hii inawezakuwa fursa ya kupata pesa za ufadhili kwa shirika hilo.



MFANO UFUATAO NI KUTOKA U.K.

Majaribio yetu yameonyesha kuwa matumizi ya UrbanFarm kibiashara yanaweza kuwa na faida. Kwa mfano, huko Uingereza mfuko mmoja wa plastiki, mbolea na mbegu iliyopandwa ya Nyanya hugharimu takriban KSH 61 kwa begi moja. Mfuko wa wastani utatoa kilo mbili na nuzu za nyanya katika msimu mmoja. Bei nyanya mwaka huu (2013) KSH 520 kwa kilo. Katika hali hii uwekezaji wa KSH 61 utarudisha KSH 1300 kwa hivyo hii ina faida nzuri kibiashara na pia kwa ufadhili wa hisani.

Kumbuka mfano ulioko hapo juu ni wa msimu mmoja wa joto huko U.K. Katika nchi nyingi zinazojiendeleza msimu wa ukuzaji wa UrbanFarm ® unawezaendelea kwa kipindi kirefu, zaidi kwa mwaka mmoja na mavuno yatakuwa zaidi ikilinganishwa na mfano huu kutoka U.K.