Rochdale Rotary Club
Rochdale Masonic Buildings
Richard Street
Rochdale
OL11 1DU
contactus@accessible-edibles.org
Tovuti hii ina habari yote unayohitaji kukuza chakula kwa gharama ya chini kabisa, kwa wakati shamba linalofaa ukulima halipatikani, na haswa kukiwa na uhaba wa maji. UrbanFarm ® hukuza mboga na matunda kwenye mifuko iliyo ning’inizwa wima ila kwa njia ya asilia.
britain
kenya
bangladesh
This video is all about our urbanfarm project:

UPATIKANANJI WA VYAKULA. JE, SHIDA NI GANI?

  1. Idadi ya watu duniani ifikapo 2050 itakuwa Bilioni 9. Kwa sasa (2013), hii idadi ni zaidi ya Bilioni 7.
  2. Ukosefu wa ajira - Ulimwenguni siku zote kutakuwa na ongezeko la idadi ya watu.
  3. MJimiatokeo yake itakuwa ukosefu wa vyakula vya kutosha.

Kuna suluhisho kwa shida zilizo hapo juu. Jibu ni kilimo cha hali ya juu kisicho tegemea ardhi ya kawaida kwani inaendelea kuadimika, tena kwa kutumia njia rahisi inayoweza kuhamishwa na kutunzwa na wakulima wasio na ujuzi wa hali ya juu mijini. Wanaweza kuwa wamejiajiri, au waajiriwa kwa mashirika yasiyo ya kiserikali, au kwa Biashara.

Ni dhahiri kuwa ukuzaji wa vyakula kwenye mifuko inayoning’inia kwa wima ya “UrbanFarm ®” haina tofauti na ukuzaji wa vyakula kwenye vikapu vinayoning'inia. Cha muhimu kwa kufaulisha mradi ni jinsi ambavyo mradi unatekelezwa.MANUFAA YA KUTUMIA URBANFARM

Kwa miaka nne iliyopita tumekuwa tukiendeleza mradi wetu wa UrbanFarm. Hii ni njia rahisi sana ya kupanda mboga na matunda katika mifuko iinayoning'inia kama huna ardhi ya ukulima.

Tuliibuni haswa kwa matumizi katika maeneo ya ukame kwani inahitaji tu viwango vidogo vya maji kuitunza. Tumefanya majaribio ya mradi huko Uingereza, Kenya na Bangladesh na matokeo yake iliridhisha kwa kuwa gharama pekee ni bei ya mbegu ambayo mara nyingi inaweza kutolewa bure na mashirika ya maendeleo.

Tafadhali angalia orodha hii ya faida na uone ikiwa unaweza kutumia UrbanFarm kwenye mradi wako. Ikiwa unahitaji msaada wowote au ushauri tafadhali wasiliana nami Mike Tomkinson at: contactus@accessible-edibles.org

Ujumbe juu ya ushiriki wa Rotary - mradi huu ulibuniwa na kuendelezwa kwa kipindi cha miaka minne na majaribio na utafiti ukafanyika Bangladesh, Kenya na Uingereza. Maendeleo yake ni nzuri na unaongozwa na Kilabu cha Rotary cha Rochdale.

Bonyeza hapa kupata mwongozo wetu utakaokusaidia kukuza chakula chako mwenyewe.